1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya mambo huko Gaza

Mutasa Omar25 Mei 2007

Israel inaendelea kuhujumu vituo vya wapalatina katika Gaza

https://p.dw.com/p/CHDk
Makombora ya Israel dhidi ya Gaza
Makombora ya Israel dhidi ya GazaPicha: AP

Kwa muda wa siku Tisa mfulilizo ndege za kijeshi za Israel zimeendelea kuushambulia mji Gaza ,licha ya mwiito wa Rais wa Palastine Mahmoud Abbas, kutaka pawepo usitishaji wa mapigano.

Mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo inasemakana baadhi ya makombora ya Israel yalianguka karibu na nyumba ya waziri mkuu wa Palastina Ismail Haniyya.

.

Ndege za kijeshi za Israel usiku wa kuamkia leo, zilifanya mashambulizi saba 7 na kuyaharibu majengo kadha, pamoja na vituo vinavyotumiwa na wapiganaji wa kundi la

Hamas,ambao ndio washirika waku, katika Serakali ya muungano ya Palastine .

Waku wa Afia katika eneo hilo,kunako kambi ya wakimbizi ya Shati, wanasema watu watano walijeruhiwa katika mashambulizi hayo, huku makombora mengine, yakiripua kijumba cha mlinzi karibu na nyumba ya waziri mkuu wa Palastine Ismael Hanniya.

Wakazi wa eneo hilo wanasema makombora hayo ya Israel, yalikua yamelengwa kuipiga nyumba ya waziri mkuu, Ismael Hanniya, lakini Jeshi la Israel limekanusha habari hizo.

Siku tatu zilizopita, waku wa Israel walitoa onyo kali kwa viongozi wa Hamas kwamba watawashambulia wapiganaji wa Hamas pamoja viongozi wao ,ikiwa wapiganaji wa Hamas, hawatoacha mchezo wao wa kuvurumisha makombora ndani ya Israel.

Tayari viongozi wa Hamas 33 akiwemo waziri wa Elimu wa Palastina, walikamatwa usiku wa kuamkia jana .

Israel inasema kwa muda wa saa 24 zilizopita

Wapiganaji wa kipalastina walivurumisha makombora zaidi ya 19 , Manane kati ya hayo kuanguka ndani ya Israel karibu na kituo cha usafiri cha EREZ kinachopakana na eneo la ghaza.

Licha ya mapigano haya kuendelea baina ya wapalastina na wa Israel ,Rais Mahmoud Abbas wa Palastina amekua akiwasihi wapiganaji wa kipalastina kusitisha hujuma zao dhidi ya Israel.

Rais Mahmoud Abbas alisema, hatutaki uvurumishaji wa makombora hayo ndani ya Israel, na lazima yakomeshwe ili tuweze kufikia makubaliano ya kuweka chini silaha, pande zote mbili, katika mji wa Gaza na Ukingo wa magharibi.

Rais Abbas aliyasema hayo baada ya kukutana na mwakilishi mkuu wa siasa ya njee ya umoja wa ulaya, Javier Solana.

Wizara ya Afia ya Palastine inasema tangu siku 10 mashambulizi ya Israel yaanze ndani ya Gaza karibu watu 38 wameuwawa Na wengine zaidi ya watu 150 kujeruhiwa.

Nayo Israel inasema, zaidi ya mokombora 220 yamepigwa kusini mwa Israel, katika kipindi hicho, mengi ya makombora hayo yakiwa ya wapiganaji wa kundi la Hamas, ambapo Mwanamke moja wa Israel ndie alieripotiwa kuwawa.