1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali Myannmar bado ni mbaya

18 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E23N

YANGOON

Waziri mmoja wa Uingereza aliyeko mjini Yangoon kwa lengo la kuushinikiza utawala wa kijeshi kuchukua hatua zaidi kuwasaidia wahanga wa kimbunga amefahamisha kwamba shughuli za kugawa misaada zimeanza kupiga hatua.Lord Malloch Brown amesma kwamba kiasi cha asilimia 25 ya wahanga wamepokea msaada wanaohitaji.Matamshi hayo yamekuja saa chache kabla ya kuwasili nchini Myanmmar mratibu wa misaada ya dharura wa Umoja wa mataifa John Holmes kwa lengo la kuzungumza na utawala huo juu ya shughuli za kugawa misaada.Holmes amepeleka pia ujumbe wa barua wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon kwa kiongozi wa Myanmar Than Shwe ambaye amekataa kuzungumza kwa njia ya simu na katibu mkuu.Shirika la kimataifa la kuwasaidia watoto la Save the Chaildren limesema kwamba kuna watoto 30,000 wanaokabiliwa na utapiamlo na kuna kitisho cha watoto hao kufariki kutokana na njaa.