1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hakuna dawa mjarabu ya matatizo ya madeni ya eneo la euro

Sekione Kitojo1 Februari 2012

Magazeti ya Ujerumani yanazungumzia mkutano wa kilele wa viongozi wa Umoja wa Ulaya, majadiliano kuhusu Syria katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na mkutano wa ujumuisho nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/13u7c
France's President Nicolas Sarkozy, left, Germany's Chancellor Angela Merkel, center, and Italy's Prime Minister Mario Monti speak together prior to a meeting at the European Council in Brussels ahead of the European Union leaders summit, Monday, Jan. 30, 2012. European leaders were trying Monday to come up with ways to boost economic growth and jobs, which are being squeezed by their own governments' steep budget cuts across the continent. (Foto:Philippe Wojazer, pool/AP/dapd) FRANCE MAGS OUT
Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy kushoto, akiwa pamoja na kansela wa Ujerumani Angela Merkel katikati na waziri mkuu wa Italia Mario Monti.Picha: dapd

Kuhusu mkutano wa umoja wa Ulaya mjini Brussels, gazeti la Westfälische Nachrichten limeandika.

Nchi za umoja wa sarafu ya euro bado hazijapata utulivu. Hatua za kubana matumizi zinaelekea kuwa kama mauaji yaliyotokea katika enzi za zamani sana zama za giza. Nchi hizi zinazungumzia kuhusu kuzuwia tatizo hilo, lakini hakuna hali ya kupona. Ni dhahiri kuwa Ugiriki inapaswa kubana matumizi. Hii itawezekana tu iwapo , dawa inayotolewa ni sahihi. Eneo la mataifa ya euro linahitaji mpango kamambe wa uwekezaji, nafasi za kazi kwa watu wake, na sio mipango nusu nusu ya ukuaji wa uchumi, kama iliyowekwa katika mkataba kuhusu udhibiti wa bajeti za nchi hizo.

Nalo gazeti la Donaukurier likizungumzia kuhusu mkutano huo wa umoja wa Ulaya linaandika:

Iwapo makubaliano katika mkutano wa kilele mjini Brussels yalikuwa kweli ni kazi ya kupigiwa mfano , kama Merkel alivyomaanisha , ni lazima kwanza matokeo yaonekane. Kwasababu katika hali ya sasa ya mzozo wa madeni , pamoja na matatizo yake yaliyojificha , haionekana hali hiyo kuondoka kama inavyoelezwa na mataifa ya umoja wa Ulaya. Hiki si kingine bali ni mabadiliko kuelekea katika hali ya wasi wasi wa maisha ya baadaye. Hadi sasa utekelezaji wa makubaliano hayo utakuwa hewa tu. Hii ni njia tu ya kuwatuliza wenye hisa katika masoko , ili kuweza kuhimiza uwekezaji barani Ulaya. Swali ni kuwa mbinu hii inafanyakazi? anauliza mhariri wa gazeti hilo.

Baraza la usalama la umoja wa mataifa linajadili azimio kuhusu Syria lililowasilishwa na mataifa ya umoja wa Kiarabu. Gazeti la Braunschweiger Zeitung kuhusu mada hiyo linaandika.

Mzozo nchini Syria unapaswa kutatuliwa na nchi hiyo binafsi pamoja na mataifa ya Kiarabu. Gharama ni kubwa, kwasababu utawala wa Bashar al-Assad bila huruma unapambana na watu wanaoupinga. Hata hivyo ghasia hizo zinapaswa kufikia mwisho. Iwapo kiongozi huyo wa Syria ataendelea kubaki madarakani , hakutakuwa na mwisho katika mzozo huu.

Umoja wa Mataifa ya kiarabu umeamua kupambana na hali hii, kwa mara ya kwanza katika historia umeonyesha kuwa umoja huo si jukwaa lisilokuwa na uwezo kupambana na madikteta, badala yake mataifa hayo yanataka kuonyesha uwajibikaji wao.

Kuhusu mada hiyo hiyo gazeti la Der Neue Tag linaandika.

Kauli nzito kutoka kwa waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle na mwenzake wa Marekani Hillary Clinton haziwezi kuiweka hali kuwa nzuri , kwasababu baraza la usalama kuweza kutoa kauli moja dhidi ya syria ni hali ambayo haiko karibu.

Berlin/ Aussenminister Guido Westerwelle (FDP) gibt am Montag (28.11.11) im Auswaertigen Amt in Berlin ein Pressestatement. Foto: Paul Zinken/dapd // Eingestellt von wa
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Guido Westerwelle .Picha: dapd

Mada nyingine hii leo ni kuhusu ujumuisho wa wageni katika jamii ya Wajerumani. Gazeti la Leipziger Volkszeitung linaandika.

Kunakosekana kina Özil katika idara za serikali, akina Boateng katika ulinzi. Kama ilivyo katika timu ya taifa ya Ujerumani , wachezaji ambao ni watoto wa wahamiaji si tu wamejumuika katika jamii, lakini pia wameleta nguvu mpya katika timu ya taifa, kwa hiyo ni lazima wajumuishwe pia kama maafisa wa idara za serikali , waalimu, na hata jeshi la polisi. Hili haliwezi kutolewa amri na mkutano wa ujumuisho. Hata kuweka sheria ya idadi maalum, hii itakuwa mbali na hali halisi duniani. Hali hii inakuja yenyewe, iwapo itaonekana kuwa ni lazima. Hali hiyo inakosekana hususan katika eneo la Ujerumani ya mashariki.

ARCHIV - Mario Götze und Mesut Özil (r) freuen sich am 02.09.2011 auf Schalke in Gelsenkirchen, nachdem sie das Qualifikationsspiel Deutschland - Österreich für die kommende Europameisterschaft EURO 2012 gewonnen haben. Bundestrainer Löw plant für die letzten Länderspiele des Jahres die Premiere für den gemeinsamen Auftritt von Özil und Götze in der deutschen Fußball-Nationalmannschaft. Foto: Roland Weihrauch dpa (zu dpa 0644 «Löw: Premiere Özil/Götze - Debüt für Zieler» vom 06.11.2011) +++(c) dpa - Bildfunk+++
Mesut Özil mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani ambaye anaasili ya Uturuki .Picha: picture alliance/dpa

Nalo gazeti la Neue Osnabrüker Zeitung linasema kuwa: Mkutano wa kilele wa tano wa ujumuisho haukuwa kikao cha burudani tu ya kunywa kahawa kama baadhi ya wakosoaji wanavyosema . Walioshiriki wameondoka katika mkutano huo na mpango maalum wa kitaifa unaopaswa kuchukuliwa hatua. Na katika hili serikali ya Ujerumani imo katika njia iliyo sahihi. Wageni wengi wanapaswa kupatiwa kazi katika nyanja muhimu katika jamii. Wengi wao wanapaswa kuajiriwa katika sekta ya umma na kutambuliwa kwa viwango vyao vya elimu na lugha. Huo ni mfano mzuri.

Mwandishi: Sekione Kitojo/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman