1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki za binadamu zinakiukwa kwa madai ya kupambana na ugaidi.

6 Agosti 2008

Jopo la wataalamu limesema nchi wanachama wa umoja wa mataifa wanapuuzia sheria za kimataifa za haki za binadamu.

https://p.dw.com/p/ErkQ

Jopo la wataalamu limesema nchi wanachama wa umoja wa mataifa wamekuwa mara kwa mara wakipuuzia sheria za kimataifa za haki za binadamu na misingi yake kwa jina la kupambana na ugaidi.

►◄

Ugunduzi huo uliopewa jina la ngome ama kasri la mchanga? haki za binadamu katika enzi za kupambana na ugaidi, ilikuwa ni sehemu ya saba ya mfululizo wa mdahalo mpya wa haki za binadamu, mfululizo wenye sehemu 12 kila mwezi kwa kumbukumbu ya mwaka wa sita wa maandhimisho ya tangazo la kimataifa la haki za binadamu.

Vifungu 30 vya tangazo la kimataifa la haki za binadamu, likisomwa hii leo ni kama orodha ya matusi, na mara nyingi uendeaji kinyume haki za binadamu unaofanywa kwa jina la kile kinachoitwa kupambana na ugaidi , amesema Craig Mokhiber , wa ofisi ya umoja wa mataifa ya haki za binadamu, ambaye alikuwa msimamizi katika jopo hilo.

Baadhi ya maeneo yanayotia shaka kwa mujibu wa mapambano dhidi ya ugaidi yaliyosisitizwa na wajumbe wa jopo hilo ni upanuzi wa madaraka ya polisi, matumizi ya mahakama za siri na ushahidi, matumizi ya sheria ya kuwekwa kizuizini, na hukumu ya kifo kwa makosa ambayo hayakusababisha mauti.

Sheria za kupambana dhidi ya ugaidi zilizopitishwa duniani kote zimewakilisha upanuzi mkubwa wa madaraka ya serikali katika kuchunguza, kuweka kizuizini , kuhukumu na kumfunga mtu kukitumika mwelekeo finyu wa kisheria, uwazi na hatua zinazostahili za kisheria, amesema Joanne Mariner, mkurugenzi wa mpango wa mapambano dhidi ya ugaidi wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Sheria hizi zinabana haki ya magaidi, wapinzani kisiasa, wanaharakati wanaotetea masuala ya jamii na wahalifu wa kawaida, kwa mujibu wa Mariner.

Sheria hizo ni sehemu ya matokeo ya kukosekana kwa ufafanuzi wa kimataifa wa ugaidi, ambao bila huo nchi zinaruhusiwa kujenga hoja binafsi juu ya kile kinachoitwa makundi ya kigaidi ama tukio la kigaidi. Ukiukaji wa haki za binadamu unaotokana na sheria hizo uko katika misingi, unaongezwa na mbinyo wa kimataifa kutoka kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuwa mataifa wanachama yaonyeshe kuwa yanapambana na ugaidi katika nchi zao.

Marekani miongoni mwa mataifa mengine imejaribu kuhalalisha ukiukaji wa baadhi ya sheria za kimataifa za haki za binadamu kwa kudai kuwa vita dhidi ya ugaidi ni aina mpya ya mizozo ya kivita ambayo iko nje ya sheria za kimataifa za haki za binadamu na kuhitaji kuundwa kwa mfumo mpya wa sheria za kiutu.

Margaret Satterthwaite, mkurugenzi mwenza wa kliniki ya kimataifa ya haki za binadamu katika kituo cha haki za binadamu na sheria za dunia cha chuo kikuu cha sheria cha mjini New York, amedokeza kuwa, dai hili limekataliwa na mahakama kadha za juu katika mataifa kadha wanachama wa umoja wa mataifa na hata kama mahakama moja itakubaliana na madai kama hayo, mtu bado atakuwa chini ya sheria na misingi ya haki na binadamu za kimataifa za sheria mama wakati akitengeneza sheria hizo mpya.