1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Haki kabla amani ?

5 Machi 2009

Waranti wa Mahkama ya kimataifa ya Uhalifu kwa Albashir.

https://p.dw.com/p/H6PF
Omar al-BashirPicha: picture-alliance/ dpa

Mahkama Kuu ya Kimataifa juu ya Uhalifu wa Vita mjini The Hague,Uholanzi,kwa mara ya kwanza i imetoa hati ya kukamatwa kiongozi alie madarakani-Rais Omar Al Bashir wa Sudan. Hatua hiyo lakini, haiwezi kuchukua nafasi ya siasa isioregarega mbele ya Sudan-anadai Ute Schaeffer,mkuu wa Idhaa za kiafrika wa Deutche welle katika uchambuzi wake:

Maalfu ya waandamanaji waliandamana mjini Khartoum Jumatano kupinga hati hiyo ya Mahkama Kuu ya Kimataifa kuhusu uhalifu dhidi ya Rais Omar Al-Bashir.Kiasi cha nchi darzeni 3-nyingi zikiwa za kiafrika, zikatishia kuacha kuitambua Mahkama hiyo,kwahivyo kisa hiki cha Al-Bashir, kinatishia kuzusha changamoto katika jamii ya kimataifa.

Orodha ya nchi ambazo haziungi mkono moja kwa moja Mahkama hiyo itaongezeka na kuwa ndefu.Hadi sasa orodha hiyo ikijumuisha tu Marekani,Urusi,India,Pakistan,China,Israel na Iran.Hata wakaazi wa Sudan wataona athari za kutolewa hati hiyo .Kwsani, hati hiyo itazidi kuchafua hali mbaya ya kibinadamu iliopo Sudan,kwavile Sudan imeyataka mashirika ya utoaji misaada kufunga virago na kuondoka nchini. Isitoshe, itacharibu juhudi za kuleta amani nchini.Kikundi kimoja cha waasi mkoani Dafur,kutokana na kutolewa hati hiyo ya kukamatwa kwa Bashir,kimeshajitoa katika mazungumzo ya amani.Zaidi hati hiyo itaitenga nchi hii ambayo tayari inatuhimiwa kutoa kinga kwa magaidi wa kiislamu.

Hati hii ni ya kwanza kuamrisha kutiwa nguvuni kwa rais alie madarakani na inazusha swali la kimsingi: Je, yawezekana kuleta haki kabla ya kwanza kuleta amani ?

Jibu ni la, kwa muujibu zionavyo Taasisi kama vile Umoja wa Afrika na nchi ambazo zinazopaswa kuelewa hali ilivyo: mfano Ruanda,Yugoslavia ya zamani au Afrika Kusini.Ni baada ya kwanza kufikiwa amani ,baada ya kumalizika vita na mauaji ya kimbari ,ndipo waliohusika wanapohukumiwa.

Hakuna shaka kuwa Rais Al Bashir anabeba jukumu kwa jicho la Mahkama hiyo inayochunguza mauaji ya halaiki,uhalifu dhidi ya wanadamu na kukanyagwa haki za mwanadamu na madhambi ya vita.Ssali lakini kwanini imeamuliwa sasa ? na je, hati ya kukamatwa ni chombo barabara cha kutumika kukomesha vita na matumizi ya nguvu nchini Sudan ?

Hapa kunazuka shaka shaka.Kungelikuwa na njia nyengine nyingi za kufuatwa ,lakini Jumuiya ya kimataifa haikutaka kujitwika jukumu mfano kuweka vikwazo vikali vya UM ,shinikizo tangu la kisiasa hata la kiuchumi kutoka kwa washirika muhimu wa kibiashara na usoni kabisa China. Na kwanini nchi za magharibi zingali bado zinauza silaha Sudan ikiwa zinataka amani ?

Hakuna anaetaka kuwa na hali ya kutowajibika ki- sheria sio ulimwengu wa kiarabu wala Umoja wa Afrika ulioikosoa hati hiyo ya kukamatwa Al Bashir.

Na hii bila shaka, ni hoja nzito:Hakuna adhabu inayoweza kupitishwa katika nchi yenye ugomvi kama Sudan ambako kuna migogoro kadhaa ya kimkoa na ambayo taasisi zake za kisiasa ni dhaifu na umma haushirikishwi katika maamuzi -umma ambao mwaka huu unakabiliwa na uchaguzi muhimu. Hii ni Mahkama ambayo ina uwezo tu wa kutoa waranti bali haimudu kuutekeleza binafsi bali inategemea ushirikiano wa nchi zilizoguswa na kisa hiki.