GUSAU :Watu 40 wahofiwa wamekufa nchini Nigeria | Habari za Ulimwengu | DW | 01.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GUSAU :Watu 40 wahofiwa wamekufa nchini Nigeria

Watu 40 wanahofiwa kuwa wamekufa baada ya bwawa kusambaratika nchini Nigeria.

Habari zinasema nyumba karibu 500 zilifagiliwa mbali na maji kwenye mji wa Gusau katika jimbo la Zamfara kaskazini mwa nchi hiyo.

Gavana wa jimbo hilo amesema kuwa bwawa limepasuka kutokana na mvua kubwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com