1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gordon Brown hatahudhuria mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na Afrika

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTz5

Waziri mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, amesema hatahudhuria mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na bara la Afrika utakaofanyika mjini Lisbon nchini Ureno tarehe 8 na 9 mwezi ujao.

Brown ameamua kutoshiriki kwenye mkutano huo baada ya rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, kusema atahudhuria mazungumzo hayo ya mjini Lisbon.

Gordon Brown amesema hayuko tayari kukaa meza moja na rais Mugabe ambaye amekuwa akiitawala Zimbabwe tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mnamo mwaka wa 1980 na anayeshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu.

Ureno, inayoshikilia urais wa Umoja wa Ulaya, imekosolewa vikali kwa kumualika rais Mugabe, lakini viongozi wa Afrika wamesema hawatahudhuria mkutano wa mjini Lisbon iwapo rais Mugabe hataruhusiwa kuhudhuria.