1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gordon Brown atangaza kutokwenda Ureno kwenye mkutano wa Afrika na Ulaya

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTor

LONDON.Waziri Mkuu wa Uingereza Gordon Brown amesema kuwa hatoudhuria mkutano wa kilele kati ya wakuu wa afrika na Ulaya utakaofanyika tarehe 8 na 9 mwezi ujayo huko Ureno.

Brown amesema hayo baada ya Rais Robert Mugabe kunukuliwa akisema kuwa atahudhuria mkutano huo Lisbon.

Waziri Mkuu huyo wa Uingereza amesema kuwa haiwezekani kwao kuhudhuria mkutano huo na kukaa pamoja na Mugabe.

Rais Mugabe anatuhumiwa na nchi za magharibi zikiongozwa na Uingereza kwa kile zinachosema uvunjaji wa haki za binaadamu na demokrasia.

Umoja wa Ulaya umemuwekea vikwazo vya kusafiri kiongozi huyo wa Zimbabwe.