1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gordon Brown afungua soko la hisa la Uingereza mjini Beijing

18 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CuHX

Waziri mkuu wa Uingereza Gordon Brown amefungua soko la hisa la Uingereza mjini Beijing, huku akiwa ziara yake ya siku tatu nchini China inayolenga kupanua biashara kati ya nchi hizo mbili.

Gordon Brown amesema soko hilo litasaidia kuboresha biashara na uwekezaji kati ya China na Uingereza na kuzisaidia kampuni za China kunufaikia katika soko la hisa la mjini Uingereza.

Bwana Brown pamoja na mwenyeji wake waziri mkuu wa China, Wen Jiabao, wametangaza kwamba wanalenga kuongeza biashara kwa asilimia takriban 50 inayonuiwa kufikia thamani ya dola bilioni 60 ifikapo mwaka wa 2010.

Gordon Brown pia ameanza juhudi za kuvutia uwekezaji zaidi wa China nchini Uingereza.

Maswala mengine katika ajenda ya waziri mkuu Gordon Borownf katika ziara yake nchini Chin ani pamoja na usalama wa kimatiafa, mazingira na swala la haki za binadamu.