1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

180111 Nigeria Wahlkampf

18 Januari 2011

Vyama vya kisiasa nchini Nigeria mwishoni mwa juma lililopita viliteua wagombea wake katika uchaguzi ujao wa rais mwezi wa Aprili. Chama tawala cha PDP kimemteua Goodluck Jonathan.

https://p.dw.com/p/zzJe
RaisGoodluck JonathanPicha: AP

Mwishoni mwa juma lililopita, vyama vyote vya kisiasa nchini Nigeria vilitakiwa kisheria kuwasilisha majina ya wagombea wao wa kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Aprili. Nchi hii, yenye wakaazi wengi katika bara la Afrika, inajiweka tayari pia kwa mara ya nne kufanya uchaguzi wa baraza la wawakilishi. Rais aliyeko madarakani Goodluck Jonathan, kutoka jimbo linalozalisha mafuta kwa wingi la Niger-Delta, amefanikiwa kuendelea kuwa kiongozi wa chama tawala cha PDP. Hasimu wake kutoka eneo la kaskazini ya nchi hiyo, Atiku Abubakar, ameshindwa vibaya na Jonathan.

Oelanlagen in Nigeria
Jimbo la Niger-Delta lina utajiri mkubwa wa mafutaPicha: AP

Kwa hakika baada ya kifo cha rais Umaru Yar' Adua, ambaye ni Muislamu mwanzoni mwa mwaka 2010, kungekuwa na Muislamu mwingine anayefuata. Kwa sababu ametumikia tu kipindi kimoja, kwa kawaida wanabadilishwa marais wa Nigeria kila baada ya vipindi viwili vya utawala , rais Mkristo na kisha Muislam. Makamu wake wa wakati huo , ambaye hivi sasa ndio rais Goodluck Jonathan , amebadilisha utaratibu huo. Kwa hivi sasa yeye ndie kiongozi wa chama hicho tawala cha demokrasia ya wananchi, kwa kifupi PDP. Kwa jimbo ambalo anatoka , la Niger-Delta lenye utajiri mkubwa wa mafuta, itakuwa ni mara ya kwanza , kutoka rais aliyechaguliwa. Wengi katika jimbo hilo wanafurahia jambo hilo, kama anavyoeleza mwandishi habari Peace Sinclair.

"Kwa kuwa sasa rais atatoka upande wa kusini, na kwamba anatoka miongoni mwa kabila dogo la jimbo la Niger-Delta, ni jambo tunalolikaribisha, tunafuraha, mimi nimefurahi. Na naamini kuwa mambo makubwa zaidi yatatokea nchini Nigeria. Na naamini kuwa suala la kukandamizwa litapatiwa ufumbuzi nchini Nigeria, hususan katika jimbo la Niger-Delta".

Klaus Pähler kutoka katika wakfu wa Konrad-Adenauer katika mji mkuu wa Nigeria Abuja anadhani, kuwa Peace Siclear na wakaazi wengine kutoka jimbo la Niger Delta wanafurahia kuchaguliwa kwa Jonathan kama rais. Kama kawaida chama tawala cha PDP ndio chama ambacho kimejijenga vyema katika nchi hiyo. Kwa uteuzi wa Jonathan kuwa mgombea wa chama hicho matokeo tayari yanajulikana.

Matumaini ya kaskazini yako kwa Buhari

Nigeria Wahlen Muhammadu Buhari Oppositionsparteiführer ANPP
Mgombea wa chama cha CPC, Muhammadu BuhariPicha: AP

Katika eneo la kaskazini la Nigeria wanaweka matumaini yao sasa kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi, Muhammadu Buhari. Matumaini haya anayaona pia Klaus Pähler kuwa ya kweli.

"Binafsi anaonekana kuwa si fisadi, na yuko karibu na watu wake. Na wengi wa Wanigeria wanaamini hivyo, na nchi hiyo inahitaji mtu wa aina hiyo. Kwa hiyo Buhari anaweza kuwa na nafasi, iwapo wapiga kura wengi kutoka kaskazini watampa kura zao".

Buhari katika mwaka 1983 aliingia madarakani kupitia mapinduzi akipinga rushwa na ufisadi na kuiangusha serikali ya kiraia na kwa muda wa miaka karibu miwili alitawala kwa mkono wa chuma. Baada ya kuchaguliwa kuwa kiongozi wa chama chake cha Congress for Progresive Change, CPC, Buhari alisema katika mahojiano na Deutsche Welle kuwa sasa ataanzisha demokrasia sahihi na matakwa ya wananchi , uamuzi wao dhidi ya majaribio ya udanganyifu kuulinda.

Wahlen in Nigeria Warteschlange
Wanigeria wanatarajiwa kupiga kura mwezi ApriliPicha: AP

"Kwa wakati huu tunaamini kuwa inawezekana, na tunatiwa moyo, na hali ya kujiamini miongoni mwa wananchi".

Mbali ya eneo hilo la kaskazini, Buhari haungwi sana mkono , wanaeleza wadadisi wa mambo. Mgombea mwingine muhimu ni Nuhu Ribadu. Anakiongoza chama ambacho kina nguvu upande wa kusini magharibi ya nchi hiyo cha Action Congress, kwa ufupi ACN katika uchaguzi huo wa rais. Ribadu, chini ya rais Olusagun Obasanjo, alijijengea jina kama mtu aliyepambana sana dhidi ya rushwa na ufisadi. Hussaini Abdu kutoka shirika la maendeleo, Action Aid, anafikiri kuwa Ribadu wanaweza kufanyakazi pamoja na Buhari.

"Googluck anaweza kuangushwa. Naweza kusema kuwa ama Buhari ama Nuhu Ribadu wanaweza kuingia madarakani. Mazungumzo kuhusu muungano baina ya ACN na CPC yanaendelea. Kwa hiyo kuna uwezekano, kwamba mmoja wao anaweza kuingia madarakani".

Licha ya kuwa kuna mvutano mkubwa katika chama cha PDP kuhusiana na nani wa kukiongoza chama hicho , inawezekana pia nchi hiyo itajikuta katika wiki chache zijazo katika msukosuko wa kisiasa, anahisi Abdu. Mwezi Oktoba na mwishoni mwa mwaka jana kumekuwa na mashambulio ya mabomu na kuutikisa mji mkuu wa nchi hiyo Abuja.

Mwandishi : Thomas Mösch / ZR / Kitojo Sekione
Mhariri : Othman Miraji