GHAZNI:Mateka walioachiwa wakabidhiwa kwa ICRC | Habari za Ulimwengu | DW | 29.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GHAZNI:Mateka walioachiwa wakabidhiwa kwa ICRC

Mateka wa kike watatu wa Korea kusini walioachiwa na kundi la Taleban wamekabidhiwa kwa shirika la msaada la Msalaba mwekundu Redcross nchini Afghanistan.Kwa mujibu wa mwakilishi wake nchini humo Craig Muller shirika lake limewapokea wanawake hao.

Kulingana na mwandishi wa habari wa shirika la AFP wanawake hao walijifunga mitandio na walionekana kuwa wanalia.Taarifa za kuachiwa kwao zilitolewa jana jioni jambo lililowapa ahueni jamaa zao waliokuwa wakisubiri kwa muda mrefu tangu wakamatwe.

Serikali ya Korea Kusini kwa upande wake inaahidi kuondoa majeshi yake 200 yanayohudumu katika vitengo vya utabibu na uhandisi nchini Afghanistan ifikapo mwisho wa mwaka.Aidha serikali hiyo inaahidi kusitisha shughuli za kutoa misaada zinazoongozwa na makanisa nchini Afghanistan.Hata hivyo serikali ya Korea kusini imeshapiga marufuku safari ambazo hazijaidhinishwa nchini Afghanistan.

Kundi la Taleban liliwaua wanaume wawili waliokuwamo katika kundi hilo la mateka 23 waliokamatwa Julai 19 kusini mwa Afghanistan.Wapiganaji hao wanadai kuachiwa kwa wafungwa wao wanaozuiliwa katika jela nchini humo jambo ambalo serikali ilipinga kabisa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com