1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia Uingereza zaingia siku ya nne; hadi Manchester

10 Agosti 2011

Ghasia mbaya kabisa ambazo hazijawahi kutokea nchini Uingereza kwa miongo kadha sasa zimesambaa hadi mji wa Manchester na maeneo mengine ya kati nchini humo.

https://p.dw.com/p/12Dmk
Moshi na moto unaonekana ukitoka katika jengo moja katika kitongoji cha Croydon mashariki ya London jana huku polisi akiangalia .Picha: dapd

Ghasia mbaya kabisa ambazo hazijawahi kutokea nchini Uingereza kwa miongo kadha zimesambaa hadi Manchester na katika maeneo ya kati ya viwanda jana Jumanne usiku ,huku makundi ya vijana yakivunja madirisha, kupora mali na kuchoma moto majumba. Ni mara ya kwanza ghasia kama hizo kulikumba eneo la mji huo wa kaskazini magharibi ya Uingereza baada ya siku tatu za ghasia mjini London na katika maeneo mengine. Jana Jumanne, waziri mkuu David Cameron , akirejea mapema kutoka katika likizo yake, ameahidi kufanya kila linalowezekana , kurejesha utulivu katika mitaa. Kiasi ya maafisa wa polisi 16,000 kutoka sehemu mbali mbali za nchi hiyo wamekusanyika mjini London, mji ambao kwa kiasi kikubwa umetulia wakati giza lilipoingia. Mtu mmoja ambaye amekutwa amepigwa risasi katika gari wilaya ya kusini ya Croydon mjini London alifariki akiwa hospitali jana Jumanne, ikiwa ni kifo cha kwanza kutokana na ghasia hizo. Ghasia kwanza zilizuka katika eneo la Tottenham kaskazini ya London siku ya Jumamosi, baada ya maandamano ya amani yakipinga kuuwawa kwa kupigwa risasi Mark Duggan na polisi. Shirika linalochunguza matendo ya polisi ya Uingereza limesema jana kuwa halikupata ushahidi kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 29 alifyatua risasi dhidi ya polisi.

London Proteste und Ausschreitungen August 2011
Waziri mkuu wa Uingereza David Cameronameahidi kufanya kila linalowekezana kurejesha amani katika mitaaPicha: dapd