Gesi iliyopigwa maarufuku ilitumika kuwakandamiza waandamanaji katika nchi za kiarabu | Matukio ya Kisiasa | DW | 21.12.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Gesi iliyopigwa maarufuku ilitumika kuwakandamiza waandamanaji katika nchi za kiarabu

Wanaharakati wa mataifa ya Mashariki ya Kati wanadai askari wa kutuliza ghasia huenda walitumia sumu iliopigwa marufuku,katika moshi wa gesi ya kutoa machozi wakati serikali ikijaribu kuzima maandamano hivi karibuni.

A protester throws a gas canister towards Egyptian riot police, not seen, near the interior ministry during clashes in downtown Cairo, Egypt, Sunday, Nov. 20, 2011. Firing tear gas and rubber bullets, Egyptian riot police on Sunday clashed for a second day with thousands of rock-throwing protesters demanding that the ruling military quickly announce a date to hand over power to an elected government. (Foto:Tara Todras-Whitehill/AP/dapd)

Waandamanaji Misri wakitimuliwa kwa gesi ya kutoa machozi

Akielezea jinsi gesi hiyo ya kutoa machozi ilivyomuathiri, mkuu mmoja wa masoko nchini Misri, Mahmoud Hassan, amesema alijisikia dhaifu na alipatwa na kizunguzungu mara tu baada ya kuvuta gesi hiyo.

Mahmoud ambaye alikimbizwa hospitalini mwezi uliopita, kufuatia maandamano ya kuupinga utawala jijini Cairo, ameshuhudia jinsi gesi hiyo ilivyoathiri raia wengi na anakumbuka jinsi mikono yake ilivyokuwa ikitetemeka bila kukoma.

Wanaharakati wa nchini Misri wamesema gesi iliyotumika kuwatawanya waandamanaji msimu huu, ilikuwa na nguvu mara dufu ukilinganisha na ile iliyotumiwa na vikosi vya serikali ya Hosni Mubarak, dhidi ya maandamano ya siku 18 yaliyouangusha utawala wa kiongozi huyo wa kiimla.

A Protester throws a tear gas canister away during clashes with the Egyptian riot police near Tahrir square in Cairo, Egypt, Tuesday, Nov. 22, 2011. Egypt's civilian Cabinet has offered to resign after three days of violent clashes in many cities between demonstrators and security forces, but the action failed to satisfy protesters deeply frustrated with the new military rulers. (Foto:Khalil Hamra/AP/dapd)

Waandamanaji nchini Misri

Sumu hiyo iliyoko katika gesi hiyo pia iliunguza ngozi na mapafu ya waandamanaji hao. Wachunguzi wa mambo wanahisi kuwa gesi hiyo ndiyo iliyosababisha vifo vya karibu raia wanane nchini Bahrain, tangu mwezi wa Februari mwaka huu.

Madaktari wa jijini Sanaa, Yemen wamesema waandamanaji waliopelekwa hospitalini wakati wa wimbi hilo, walikuwa wamepooza na wasiojitambua, na baada ya vipimo walionekana kuathiriwa na gesi ya machozi walioivuta.

Sumu hiyo ni poda iliyotengenezwa na kemikali ya ortho-chlorobenzylidene-malononitrile, maarufu kama CS. Kemikali hiyo ilitumika katika miaka ya hamsini, kudhibiti mikusanyiko ya watu na kutokana na ukali wake, ikatafutwa kemikali nyingine mbadala aina ya chloroacetophenone CN.

Makombora ya gesi za machozi yaliyokusanywa katika maeneo yaliyofanyika maandamano katika nchi za kiarabu yana nembo za makampuni mbalimbali. Idadi kubwa ya makombora yaliyookotwa katika viunga vya Tahrir, jijini Cairo, yana nembo za kampuni ya Marekani-Combined Tactical Systems (CTS) -inayotengeneza kemikali zinazowasha na vifaa vya kijeshi kwa ajili ya majeshi ya polisi na ulinzi sehemu mbalimbali duniani.

Anti-government protesters run through clouds of tear gas late Thursday night, Aug. 11, 2011, during clashes with riot police in the Shiite Muslim village of Jidhafs, Bahrain, on the outskirts of the capital of Manama. Major protests have been crushed, but small-scale clashes have occurred nearly nightly for weeks. (Foto:Hasan Jamali/AP/dapd)

Gesi ya kutoa machozi yatumiwa kwa waandamanaji nchini Bahrain

Kwa mujibu wa maelezo ya mwanaharakati wa Shirika la Haki za Binadamu la Misri, Sherif Azer, makombora mengine yaliyookotwa katika nchi hizo za Mashariki ya Kati yana nembo za Kampuni ya Federal Laboratories and British Weapons Manufacturer Chemring yenye makao yake makuu nchini Marekani.

Kwa upande mwingine, makombora yaliyookotwa nchini Bahrain kufuatia maandamano ya mwaka huu yana nembo ya Kampuni moja ya Marekani ijulikanayo kwa jina la NonLethal Technologies.

Na wakati makampuni ya Federal Laboratories, CTS, Chemring na Kampuni ya Ulinzi ya Ufaransa, SAE Alsetex, yakiwa katika orodha ya kusambaza silaha katika nchi za Kiarabu, CTS ni kampuni inayoongoza katika kupeleka askari wa kutuliza machafuko katika serikali ya Yemeni.

Wakati wanaharakati wa haki za binadamu wakishindwa kuthibitisha tuhuma hizo, wachunguzi wengine wa mambo wanahisi vikosi hivyo vya serikali katika nchi za kiarabu walitumia gesi za machozi zilizoisha muda wake, na hiyo ndiyo sababu athari zake kwa waandamanaji zilikuwa mbaya sana.

Gesi za kutoa machozi, aina ya CS zina uwezo wa kudumu kwa kati ya miaka mitatu mpaka mitano lakini wanaharakati wa jijini Manama, Bahrain na Misri wamesambaza picha za makombora yanayoonesha kutengenezwa zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Wizara ya Afya nchini Misri imekanusha tuhuma hizo, na uchunguzi zaidi unaendelea.

Mwandishi: Pendo Paul Ndovie/IPS

Mhariri:Josephat Charo

 • Tarehe 21.12.2011
 • Mwandishi
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13XDE
 • Tarehe 21.12.2011
 • Mwandishi
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13XDE

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com