1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Germany-Georgia

Hamidou, Oumilkher23 Agosti 2008

Kansela Angela Merkel ahimiza paitishwe mkutano wa majirani za Georgia kulinda utulivu katika eneo hilo

https://p.dw.com/p/F3c7

Berlin:


Kansela Angela Merkel wa Ujerumani anapendelewa paitishwe mkutano wa kimkoa wa majirani wa Georgia.Habari hizo zimetangazwa na shirika la habari la Ufaransa AFP likimnukuu msemaji wa idara ya habari ya serikali kuu ya Ujerumani mjini Berlin.Katika toleo la jumatatu ijayo, jarida la Der Spiegel linasema kansela Angela Merkel ametoa pendekezo hilo kwa rais Nicholas Sarkozy,ambae nchi yake ndio mwenyekiti wa zamu wa Umoja wa ulaya.Urusi haijaingizwa katika orodha ya nchi zinazotazamiwa kualikwa mkutanoni-amesema hayo msemaji wa wa idara ya habari ya serikali kuu.Mkutano huo utazungumzia ujenzi mpya na  juhudi za kuimarisha utulivu nchini Georgia na katika eneo la kusini mwa Caucasus.Kansela Angela Merkel amepangiwa kuzitembelea Sweeden ,Estonia na Lithuania jumatatu na jummanne ijayo,ziara itakayogubikwa na mzozo wa Georgia na siasa ya nje ya Urusi.Viongozi wa eneo hilo wameelezea mshikamano wao pamoja na rais Mikhail Saakashvili wa Georgia.Ujerumani inajaribu kuendesha juhudi za kusawazisha hali ya mambo katika eneo la Caucasus.