1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GENEVA:Wasaidizi 4 watekwanyara Afghanistan

28 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBM2

Halmshauri ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu-ICRC imethibitisha kuwa wafanyakazi wake wanne wametekwa nyara nchini Afghanistan,kusini-magharibi ya mji mkuu Kabul.Hapo awali,msemaji wa wanamgambo wa Kitaliban aliarifu kuwa kundi hilo limewazuia wafanyakazi hao wanne.Wawili ni raia wa Afghanistan na wengine ni raia wa kigeni kutoka Burma na Macedonia.Wafanyakazi hao wa Msalaba Mwekundu,walitekwa nyara walipokuwa katika ujumbe wa kupata uhuru wa mhandisi wa Kijerumani alietekwa nyara tangu mwezi wa Julai.