1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gazetini

1 Julai 2008

Wahariri wa magazeti ya leo ya Ujerumani wamechambua pia juu ya Zimbabwe na juu ya rais wa Ujerumani .

https://p.dw.com/p/EU7W

Miongoni mwa mada zilizo chambuliwa na wahariri wa magazeti ya Ujerumani hii leo , ni uamuzi wa Rais Horst Kohler wa Ujerumani, kutotia saini Mkataba wa Lisbon wa wa Umoja wa Ulaya na maoni ya ulimwengu wa nje juu ya uchaguzi wa rais nchini Zimbabawe uliomtawaza tena kitini Rais Mugabe:

Gazeti la FRANKFURTER ALLGEMEINE ZEITUNG laandika:

"Linabaki swali kifanywe nini nchini Zimbabwe, ili uchaguzi ule wa mizengwe ufutwe na dikteta ambaye eti "amechaguliwa na umma" ashawishike alao agawane madaraka. Alao hatua hiyo ingepaswa kuchukuliwa ili kuunyima utawala huo mamlaka ya kuuwezesha kun'gan'gania madaraka inayotumia kuukandamiza Upinzani.

Gazeti lakini ,linaongeza kuwa, hata katika migogoro inayolingana na huu wa Zimbabwe,watawala waweza kutegemea marafiki wenye nguvu na sauti katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwaokoa. Kwahivyo, laandika gazeti:

: "Mpira uko katika lango la Umoja wa Afrika kuucheza.Kwa kadiri Umoja huu, hautaucheza kama timu moja ,nguvu moja na ari moja kumshinikiza Mugabe na kutochukua hatua, demokrasi ya kiini macho itaendelea na watawala kama Mugabe hawana hawatakua na cha kuogopa kuwafika."

Hilo lilikua Frankfurter Allgemeine Zeitung:

Ama gazeti la SÜDDEUTSCHE ZEITUNG laandika:

"Ni jukumu la viongozi wa Afrika kukifumbua kitandawili cha Zimbabwe.Umoja wa Ulaya unaweza tu kumsaidia mshirika wake - Umoja wa Afrika.Lakini Umoja wa Ulaya usijaribu kulazimisha mkondo na kasi ya ufumbuzi huo.

Mpango wa pamoja kati ya UA na UU kuisaidia Zimbabwe , bila ya Mugabe, ambamo Umoja wa Ulya utachangia sehemu kubwa,yamkini ukaonesha njia ya kuinusuru Zimbabwe kujikomboa kutoka balaa lake.

Sharti la msaada huo ni kuwa,kizazi kichanga cha viongozi wa Afrika kidhihirishe kimemudu kukabiliana na changamoto ya Zimbabwe."

Nalo gazeti la FINANCIAL TIMES DEUTSCHLAND linaona:

" kizazi hicho kipya cha viongozi hao kinamn'gan'ngania Mugabe madarakani kama heshima kwa kiongozi wao mkongwe na kutumbua macho tu Zimbabwe ikitumbukia shimoni au ziharakishe kumaliza udhia kwa kumpokonya nguzo anayoegemea kusalia madarakani -kuwa aliongoza vita vya ukombozi dhidi ya wakoloni."

Kwa jicho la busara ni hoja moja tu inayofahamisha hatua za pole pole zinazoudhi zinazochukuliwa-nayo ni ile kanuni ya "kutojiingiza ndani ya mambo ya nchi nyengine" ambayo ni muhimu kwa wanachama wote hata ikiwa wanawakandamiza wananchi wao.

Kuwa imesadifu ni rais wa afrika Kusini,moja ya nchi chache za kiafrika zinazofuata demokrasia ya kupigiwa mfano anazima kuchukuliwa hatua kali,inaudhi sana.Kwa Zimbabwe yenyewe huu ni msiba."

Hayo ni maoni ya FINANCIAL TIMES la Ujerumani.

Likitugeuzia mada, gazeti la THÜRINGER linauchambua ingawa kwa muhutasari tu, uamuzi wa rais wa Ujerumani Horst Kohler kuzuwia kutia saini yake Mkataba wa Lisbon wa Umoja wa Ulaya.Laandika:

"Kohler hachukui uamuzi huo kwa kuwa anautilia shaka-shaka mkataba huo wa Umoja wa Ulaya au anauona unakiuka katiba ya Ujerumani.La hasha.Ameamua hivyo kwa kuwa angetia saini, angezuwiliwa na Mahakimu wa Mahkama kuu ya Katiba mjini Karlsruhe.Kikundi cha wabunge wa mrego wa shoto kingemzima.Ili kuepuka mgongano kati ya taasisi mbili za shirikisho-Berlin na Karlsruhe, Kohler ameamua kutoa tia saini kwa sasa."