1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Hamas na Fatah wabadilishana wafungwa

31 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWQ

Makundi ya Hamas na chama cha Fatah wanabadilishana wafungwa waliokamatwa katika mapigano ya hivi karibuni yaliohusisha pande zote mbili katika Ukanda wa Gaza.Hatua hiyo ni baadhi ya makubaliano yaliyofikiwa ya kusitisha vita yaliyofikiwa jana usiku.Makubaliano hayo ya kusitisha vita yanaendelea hata baada ya kamanda mmoja wa Hamas kupigwa risasi.Kundi la Hamas linalaumu kundi la Fatah kwa kutekeleza mauaji hayo yaliyotokea mjini Khan Younis.Ghasia za hivi karibuni zimesababisha vifo vya takriban watu 30 na kuyumbisha juhudi za Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wa chama cha Fatah kuunda serikali ya kitaifa.

Rais George Bush wa Marekani anaagiza msaada wa yapata dola milioni 86 ili kuimarisha majeshi ya usalama yanayoungwa mkono na Rais Mahmoud Abbas.

Thibitisho la ahadi hiyo linatokea siku moja baada ya mpiganaji mmoja wa Kiislamu kushambulia eneo la Eilat nchini Israel kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 9.Chama cha Rais Abbas cha Fatah kinavutana na chama cha Hamas kilichopata ushindi mkubwa katika uchaguzi mwaka jana kuunda serikali ya kitaifa.

Msaada huo ni sehemu ya mpango wa Marekani wa kujaribu kufufua mazungumzo ya amani kati ya Rais Abbas na taifa la Israel.Hayo yanatokea kabla ya mkutano wa wasuluhishi wa pande nne kuhusu amani ya mashariki ya kati.Washiriki hao ni Marekani,Urusi,Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa.