1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Gaza mapigano yazidi kati ya wanajeshi wa Israel na wanamgambo

20 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBq2

Kiasi cha wanamgambo watatu wakipalestina wameuwawa ukingo wa magharibi katika mji wa Jenin kufuatia mapambano kati ya wanajeshi wa Isreal na wanamgambo.

Mapambano hayo yametajwa kuwa makali kabisa tangu kundi la Hamas kudhibiti eneo hilo wiki iliyopita.

Wakati huo huo mamia ya wapalestina wanaojaribu kukimbia machafuko katika Gaza wamelazimika kukaa usiku mwingine kwenye kivuko cha kuingia Israel cha Erez baada ya Israel kukataa kufungua mpaka wake.

Hata hivyo waziri wa ulinzi wa Israel Ehud Barak amewataka wanajeshi wa Israel kuwaruhusu wapalestina kadhaa wanaohitaji msaada wa dharura kuingia Israel.

Kufuatia hali ya hivi sasa huko Gaza waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert amesema nchi yake iko tayari kuwasaidia wapalestina.

Mahakama kuu ya Israel ilipangiwa leo hii kusikiliza ombi la makundi ya haki za binadamu la kuitaka serikali itoe huduma ya haraka ya matibabu kwa wapalestina wasiojua kwakwenda huko Gaza.