1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA.Baraza la mawaziri la Hamas kujiuzulu katika siku mbili zijazo

14 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCSU

Waziri mkuu Ismail Haniya na baraza lake la mawaziri la chama cha Hamas kinacho tawala maeneo ya Palestina watajiuzulu kutoka serikalini katika siku mbili zijazo ili kufanikisha makubaliano ya serikali ya umoja iliyoundwa kati ya vyama vya Hamas na Fatah.

Wakati huo huo Israel na Palestina zimeshindwa kuelewana juu ya ajenda zitakazojadiliwa katika mkutano uliopangiwa kufanyika wiki ijayo.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleeza Rice ilipangwa akutane na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas mjini Jerusalem wiki ijayo lakini Israel imesema kwamba inataka kwanza kujua zaidi juu ya serikali ya umoja ya eneo la Palestina.