1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Watatu wauwawa katika mapigano.

21 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7E2

Watu watatu wameuwawa katika mapigano baina ya makundi ya Wapalestina katika ukanda wa Gaza. Duru za hospitali zimesema kuwa watu 45 wamejeruhiwa. Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 51 amefariki baada ya kupigwa na risasi iliyofyatuliwa bila kulengwa mahali maalum.

Watu wawili wameuwawa, ikiwa ni pamoja na kijana mwanamume mwenye umri wa miaka 13, katika mapigano mjini Gaza , baina ya polisi wanaounga mkono chama cha Hamas na wanandugu wa ukoo wa Helles ambao wanaunga mkono chama cha Fatah cha rais wa Palestina Mahmoud Abbas. Ukanda wa Gaza umekuwa chini ya udhibiti wa Hamas tangu kundi hilo kuwaondoa mapiganaji wanaounga mkono kundi la Fatah Juni mwaka huu.