1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina wawili washambuliwa na wanajeshi wa Israel

15 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCaS

Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi la Israel, kikosi cha jeshi la Israel kimewashambulia na pengine kuwaua wapalestina wawili karibu na eneo la mpakani kaskazini mwa Ukanda wa Gaza mapema leo.

Wanajeshi wa Israel waliwafyatulia risasi wapalestina hao walipokuwa wakiukaribia mpaka wakiwa wamebeba mabomu.

Maofisa wa Palestina hawajatoa taarifa yoyote kuhusiana na hatima ya watu hao. Usitishwaji wa mapigano baina ya Israel na Palaestina ulitangazwa majuma saba yaliyopita.