1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina watano wauwawa

29 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCWn

Wapalestina watano wameuwawa usiku wa kuamkia leo kwenye machafuko yanaendelea katika Ukanda wa Gaza. Idadi ya vifo iliyosababishwa na mapigano kati ya chama cha Hamas na Fatah huko Gaza imefikia 30.

Mapigano yameendelea usiku kucha katika mji wa kusini wa Khan Younis ambako watu watatu wameuwawa. Watu wengine wawili wameuwawa mjini Gaza.

Mapigano hayo yamekwamisha juhudi za kuunda serikali ya umoja ya taifa na kuliweka eneo la Gaza katika hatari ya kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe.