Gaza: Wapalestina wafikia makubaliano mapya | Habari za Ulimwengu | DW | 04.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Gaza: Wapalestina wafikia makubaliano mapya

Vikundi hasimu vya Fatah na Hamas huko Palestina vimefikia makubaliano mapya, ambapo vitabadilishana wafungwa.

Mapema leo takriban watu watano wameuawa katika mapigano yaliyoibuka huko Gaza kati ya wapiganaji wa vikundi hivyo viwili.

Miongoni mwa waliyouawa ni maafisa usalama watatu wa Fatah huko kusini mwa ukanda wa Gaza katika mji wa Khan Younis.

Maafisa usalama wa Palestina wamewataka wageni kuondoka katika ukanda wa Gaza kufuatia vitisho vya utekaji nyara .Tayari mpigapicha wa shirika la habari la Ufaransa AFP, raia wa Peru ametekwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com