1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina 10 wauawa katika shambulio la ndege za Israeli huko Gaza

13 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3I

Wapalestina 10 wameuawa katika shambulio la ndege za Israeli katika ukanda wa Gaza. Kuna mtoto moja miongoni mwa hao waliouawa na wengine wengi ambao wamejeruhiwa, zimesema duru za utawala wa Palestina. Shambulio hilo la ndege za Israeli lililenga nyumba inayodhaniwa kuwa ya kiongozi mojawapo wa kundi lenye msimamo mkali la Hamas. Jana, wanajeshi wa Israeli waliingia na vifaru katika sehemu la kusini la Gaza kuwashambulia kwa makombora wapiganaji wa kipalestina waliokuwa huko.

Watu 6 waliuawa katika kutio hilo.