1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Umwagaji wa damu unaendelea Gaza

16 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1W

Wanamgambo wa Hamas wameua si chini ya wafuasi sita wa afisa wa usalama wa ngazi ya juu wa chama cha Fatah.Licha ya kuwepo makubaliano kati ya Hamas na Fatah kuweka chini silaha,nyumba ya afisa huyo wa usalama,ilivamiwa mjini Gaza mapema leo asubuhi.Watu wengine 10 walijeruhiwa katika shambulio hilo.Kwa mujibu wa msemaji wa Fatah, washambulizi waliitia moto sehemu ya nyumba hiyo na vile vile waliwazuia kwa muda mfupi mke na binti wa afisa huyo.Tangu siku ya Ijumaa,watu 28 wameuawa eneo la Gaza katika mapigano yaliyozuka kati ya pande mbili zinazohasimiana.Mapigano hayo yamechomza licha ya pande hizo mbili kukubali kuacha mapamabano yao kuanzia usiku wa manane wa Jumanne.Peke yake siku ya Jumapili,watu 16 waliuawa Gaza katika mapigano mabaya kupata kushuhudiwa huko Gaza.Rais Mahmoud Abbas anaekiongoza chama cha Fatah ametoa mwito wa kukomesha mapigano kati ya pande mbili hasimu.Hayo ni mapigano mabaya kabisa kupata kutokea,tangu serikali ya umoja kuundwa miezi miwili iliyopita.