1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Rais Abbas atazamia mkataba wa amani

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeu

Si chini ya Wapalestina 3 wameuawa katika shambulio la vikosi vya anga vya Israel, lililolenga gari moja katikati ya Gaza.Msemaji wa jeshi alithibitisha kuwa Israel ilifanya shambulizi la anga.Wanamgambo wa kundi la “Islamic Jihad“ wamesema,watu hao 3 walikuwa makamanda wa ngazi ya juu katika chama chao.Kwa mujibu wa ripoti za mashahidi,watu hao watatu walikuwemo ndani ya gari,lilipopigwa na kombora.