1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Mwandishi habari atekwa nyara.

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJh

Kuna taarifa kwamba mwandishi habari raia wa Uingereza ametekwa nyara katika ukanda wa Gaza. Polisi wa Palestina wamesema kuwa gari ya kukodi ya mwandishi huyo wa shirika la utangazaji la BBC imekutwa imetelekezwa katika mji wa Gaza.

Maafisa wa BBC wameeleza wasi wasi wao kwa usalama wa mwandishi huyo, lakini hawakusema lolote juu ya ripoti kuwa ametekwa nyara.

Ubalozi wa Uingereza umesema kuwa unachunguza taarifa hizo.