1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mashambulizi ya Israel yameua wanamgambo 10

6 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBlX

Hadi Wapalestina 10 wameuawa baada ya vikosi na vifaru vya Israel kuingia katikati ya Ukanda wa Gaza.Katika mapambano yaliyozuka kwenye kambi ya wakimbizi ya al-Maghazi,risasi zilifyatuliwa kati ya majeshi ya Israel na wanamgambo wa Kipalestina.Kwa mujibu wa duru za hospitali,watu wengine 13 pia walijeruhiwa katika mapambano hayo.