1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mapigano ya Hamas na Fatah yazidi kuwa makali

12 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBsQ

Makundi hasimu ya Kipalestina,Hamas na Fatah yanaendelea kupigana vikali katika Ukanda wa Gaza.Hadi watu 17 wameuawa katika mapigano mapya yaliyozuka kati ya wafuasi wa makundi hayo mawili.Miongoni mwa waliouawa ni katibu mkuu wa tawi la Fatah la kaskazini ya Gaza.Jamal Abu al-Jidian aliuawa baada ya nyumba yake kushambuliwa na wanamgambo wa Hamas.Katika shambulizi jingine nyumba ya Waziri mkuu Ismail Haniyeh wa Hamas ilipigwa na kombora lakini Haniyeh na familia yake hawakujeruhiwa.Makundi yote mawili yametumia tovuti na simu za mkono kutuma ujumbe mfupi kwa wafuasi wao,kuwahimiza kuwaua viongozi wa makundi hasimu.Wakati huo huo,wapatanishi wa Kimsri wameyahimiza makundi ya Fatah na Hamas kujadili makubaliano ya kusitisha mapigano yao.