1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Mapambano yaendelea Ukanda wa Gaza.

3 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCVb

Mapambano yameendelea kati ya makundi hasimu ya Wapalestina katika eneo la Ukanda wa Gaza na kusababisha vifo vya watu kiasi ishirini katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita.

Maafisa wa vyama vya Hamas na Fatah wamesema mwafaka mpya wa kusitisha vita umeanza kutekelezwa jana.

Rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, kwa mara nyingine tena ametoa wito vita hivyo visitishwe mara moja.

Duru zinasema, Mfalme Abdullah wa Saudi Arabia, amekuwa akiwarai Rais Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah na kiongozi wa chama cha Hamas, Khaled Mashaal wakutane juma lijalo mjini Makkah kwa mashauriano ya kutanzua mgogoro uliopo kati yao kuhusu serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina.

Mwezi uliopita viongozi hao wawili walishindwa kupatana kwenye mkutano kati yao mjini Damascus, Syria.