1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA : Jeshi la Israel lauwa wanajeshi sita

15 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZ4

Wanajeshi wa Israel wamewauwa Wapalestina sita wakati jeshi hilo lilipojipenyeza kusini mwa Ukanda wa Gaza.

Msemaji wa jeshi la Israel amesema opresheni hiyo ilikuwa imekusudia kulisaka kundi linalotuhumiwa kuwa la wanamgambo kwenye handaki na kuzuwiya wanamgambo wasifyatuwe maroketi dhidi ya taifa hilo la Kiyahudi.

Wakaazi wa eneo hilo wamesema vikosi vya Israel viliingia kwenye eneo hilo kufuatia mapambano kati ya wapiganaji wa Kipalestina na askari kanzu wa Israel.