1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Israel yashambulia tena maeneo ya Gaza.

21 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBzp

Israel imefanya mashambulizi kadha ya anga katika mji wa Gaza, kwa kujibu mashambulizi ya mara kwa mara ya makombora kutoka kwa wapiganaji wa Kipalestina.

Hapo mapema , jeshi la Israel lilirusha kombora dhidi ya nyumba moja mjini Gaza , na kuuwa wkaribu watu wanane na kuwajeruhi wengine 13.

Duru za hospitali na wakaazi wa eneo hilo zimesema kuwa nyumba hiyo ni mali ya mbunge wa chama cha Hamas Khalil al-Haya, ambaye hakuwapo nyumbani wakati wa shambulio hilo, na kwamba waliouwawa ni pamoja na ndugu zake sita.

Karakana moja inayoshukiwa kuwa inatengeneza makombora imeshambuliwa katika shambulio la pili.

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert ameapa kuongeza kasi ya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo ya wapiganaji wa Kipalestina.

Wakati huo huo makubaliano ya hivi karibuni ya kusitisha uhasama na mapigano baina ya makundi ya Kipalestina ya Hamas na Fatah yanaonekana kudumu. Kiasi cha watu 50 wameuwawa katika mapigano ya kimakundi katika muda wa wiki moja iliyopita.