1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaza. Israel yashambulia kundi la Hamas.

19 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC0n

Israel kwa mara nyingine tena imeelekeza mashambulizi yake dhidi ya kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza jana Ijumaa wakati makundi hasimu ya Kipalestina yakiendelea kupigana katika mitaa.

Watu 10 wameuwawa kwa jumla tangu Israel kuanza mashambulizi ya angani siku ya Alhamis.

Rais wa serikali ya Palestina , Mahmoud Abbas, ameitaka Marekani kuizuwia Israel kufanya mashambulizi yake.

Ismail Haniyah, waziri mkuu wa mamlaka ya Palestina na mwanachama wa Hamas , amewataka Wapalestina kuungana dhidi ya uvamizi wa Israel.

Makubaliano kadha ya kusitisha mapigano yamevunjika baina ya chama cha Hamas na Fatah cha rais Abbas katika muda wa wiki moja iliyopita na karibu watu 50 wameuwawa katika mapigano hayo.

Wakati huo huo mwandishi habari wa televisheni ya Abu Dhabi ameachiliwa huru. Televisheni hiyo imekilaumu chama cha Hamas kwa kumteka nyara Abdel Salam Abu Ashkar, dai ambalo Hamas wanalikana.