GAZA :Israel yalaumiwa kwa kupunguza usafirishaji mafuta Gaza | Habari za Ulimwengu | DW | 29.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA :Israel yalaumiwa kwa kupunguza usafirishaji mafuta Gaza

Makundi ya kutetea haki za binadamu yamepinga hatua ya Israel ya kupunguza utoaji wa mafuta kwa wakaazi wa Gaza pamoja na nia ya kutaka kukata nguvu za umeme katika eneo hilo,mashirika hayo yameonya hatua hizo huenda zikasababisha hali mbaya ya kiutu.

Makundi hayo yamepeleka malalamiko hayo mbele ya mahakama kuu ya Israel ambayo imetoa muda wa siku tano kwa serikali kujibu rufaa.Duru za Palestina zinasema Israel imepunguza usafirishaji wa mafuta ya Petroli kwa asilimia 30 katika mtambo wa pekee wa watu wa Gaza lakini msemaji katika wizara ya ulinzi ya Israel amedai wamepunguza asilimia 13 pekee ya utoaji Petroli.Israel inadai imechukua hatua hiyo kujibu mashambulizi ya roketi dhidi yake kutoka ukanda wa Gaza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com