1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Hamas yatoa orodha ya wafungwa wanaotaka waachiliwe

9 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCB7

Utawala wa Hamas katika maeneo ya Palestina umetowa orodha ya wafungwa ambao ingetaka waachiliwe na Israel kabla ya kumwachilia mwanajeshi mmoja wa Israel aliyetekwa nyara.

Orodha hiyo ilikabidhiwa wapatanishi kutoka Misri ina majina zaidi ya 1000 akiwemo kiongozi mmoja wa Fatah Marwan Barghouti.

Taarifa kutoka Israel zinafahamisha kuwa juhudi zinaendelezwa ili kumpata Koplo Gilad Shalit aliyetekwa nyara na wanamgambo wa Gaza tangu mwezi Juni mwaka 2006.

Wakati huo huo rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ametowa mwito kwa vikosi vya usalama katika Ukanda wa Gaza kudhibiti visa vya kurushwa roketi dhidi ya eneo la kusini mwa Israel.

Mpalestina mmoja laiuwawa siku ya jumamosi katika shambulio la helikopta ya Israel.

Israel imetetea hatua yake hiyo kwa kusema kuwa ililazimika kujibu mashambulio hayo ya roketi.