1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY : Serikali ya Hamas yajiuzulu kuunda serikali mpya

16 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCRm

Waziri Mkuu Ismael Haniyeh wa kundi la Hamas ametangaza kujiuzulu kwa baraza lake la mawaziri utaratibu unaotowa nafasi ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ya Palestina kwa kushirikiana na kundi la Fatah.

Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wa kundi la Fatah amemkabidhi rasmi Haniyeh jukumu la kuunda serikali mpya ya mseto.Hatua hiyo inafuatia mkutano kati ya Abbas na Haniyeh katika mji wa Gaza ambao umeitishwa kuondosha tafauti za mwisho katika makubaliano ya kushirikiana madaraka yaliofikiwa wiki iliopita.

Hata hivyo bado haijulikani iwapo serikali hiyo mpya ya umoja wa kitaifa ya Palestina itaitambuwa Israel ambalo ni dai kuu la jumuiya ya kimataifa ili kuachana na hatua yake ya kususa kuipa msaada serikali ya Palestina.