1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY: Ismail Haniyeh apona chupu chupu

21 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD0g

Waziri mkuu wa Wapalestina Ismail Haniyeh wa chama cha Hamas,amepona chupu chupu baada ya kushambuliwa katika Ukanda wa Gaza.Kwa mujibu wa Hamas,watu wasiojulikana walifyatulia risasi mlolongo wa magari ya waziri mkuu.Vikosi vya usalama vya Hamas vilimkinga Haniyeh.Wizara ya mambo ya ndani ya Wapalestina,imesema shambulio hilo limefanywa na ukoo fulani.