GAZA CITY : Haniyeh yuko tayari kujiuzulu | Habari za Ulimwengu | DW | 11.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA CITY : Haniyeh yuko tayari kujiuzulu

Waziri Mkuu wa Palestina Ismael Haniyeh wa chama tawala cha Hamas amedokeza kwamba yuko tayari kujiuzulu iwapo hatua hiyo itakomesha mataifa ya magharibi kuisusia msaada serikali yake.

Haniyeh amesema wakati suala la vikwazo likiwa upande mmoja na wadhifa wake wa uwaziri mkuu likiwa upande wa pili ni afadhali vikwazo hivyo viondolewe ili kukomesha kuteseka kwa wananchi wa Palestina.

Kauli yake inakuja baada ya mazungumzo juu ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahamoud Abbas.Hanniyeh amesema mazungumzo hayo yamekuwa yakitowa muelekeo mzuri na kwamba anatumai baraza jipya la mawaziri litaundwa katika kipindi kisichozidi wiki tatu.

Israel na mataifa ya magharibi waliiwekea vikwazo serikali hiyo ya Palestina mapema mwaka huu kutokana na kugoma kwa Hamas kuitambuwa Israel,kukanusha matumizi ya nguvu na kuheshimu makubaliano yaliopita kati ya Israel na Wapalestina.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com