1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

GAZA: Chama cha Hamas kimetishia kunyayua silaha tena

Chama tawala cha Kipalestina,Hamas kimetishia kuvunja makubaliano ya juma moja ya kusitisha mapigano kati ya makundi ya wanamgambo wa Kipalestina na Israel katika Ukanda wa Gaza. Tangazo hilo lilitolewa baada ya kutokea kifo cha kijana wa Kipalestina wa miaka 15 aliepigwa risasi na wanajeshi wa Kiisraeli.Siku ya Jumapili maroketi yaliyorushwa kutoka Ukanda wa Gaza yaliangukia ardhi ya Israel,lakini hakuna ripoti kuhusu hasara yo yote ile.Hiyo ilikuwa mara ya kumi na tano kwa Israel kurushiwa maroketi tangu kupatikana kwa makubaliano ya kusitisha mapigano.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com