1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gay na Powell kutoshiriki mashindano ya dunia Moscow

15 Julai 2013

Shirikisho la mchezo wa riadha duniani lasema mfumo wake wa kupambana na wanariadha wanaotumia madawa ya kuongeza nguvu unafanyakazi, wakimbiaji mashuhuri Tyson Gay na Asafa Powell wanasa katika mtego,wa Doping.

https://p.dw.com/p/197vI
epa03775607 Tyson Gay from the USA celebrates after winning the mens 100 m race at the Athletissima IAAF Diamond League athletics meeting in the Stade Olympique de la Pontaise in Lausanne, Switzerland, 04 July 2013. EPA/JEAN-CHRISTOPHE BOTT +++(c) dpa - Bildfunk+++
Tyson GayPicha: picture-alliance/dpa

Shirikisho la mchezo wa riadha ulimwenguni IAAF limesema kuwa kuaminika kwa mpango wake wa kupambana na wanariadha wanatumia madawa ya kutunisha misuli kumeimarika na sio kuporomoka baada ya wakimbiaji nyota Asafa Powell na Tyson Gay wa Marekani kunasa katika mtego huo baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa ya kuongeza nguvu, ambayo yamepigwa marufuku.

Gay , bingwa wa zamani wa dunia ambaye alishinda mbio za mita 100, na 200 katika mashindano ya kitaifa nchini Marekani mwezi uliopita, amesema kuwa atajitoa katika mashindano yajayo ya ubingwa wa dunia nchini Urusi mwezi ujao.

(FILE) A file picture dated 30 August 2007 shows Tyson Gay of the USA celebrating after winning the 200m final at the 11th IAAF World Championships in Athletics, Osaka, Japan. Tyson is awarded the 2007 Male World Athlete of the Year during the celebrations of the World Athletics Gala hosted by International Athletic Foundation (IAF) Honorary President HSH Prince Albert II of Monaco and IAF & IAAF President Lamine Diack in the Salle des Etoiles of the Sporting Club dÒEt- Monte Carlo, 25 November 2007. EPA/KIMIMASA MAYAMA +++(c) dpa - Bildfunk+++
Bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 na 200 duniani Tyson GayPicha: dpa

Wakabiliwa na adhabu

Powell ambaye alishikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 100 hadi Usain Bolt alipoishusha mwaka 2008, pamoja na bingwa wa medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki Sherone Simpson pia wanakabiliwa ya hatua ya kuzuiwa kushiriki michezo ya riadha baada ya kupatikana na hatia ya kutumia madawa hayo katika michezo ya chama cha riadha cha Jamaica mwezi uliopita.

FILE - In this Saturday, May 19, 2013 file photo, Asafa Powell of Jamaica, center, competes with Nesta Carter of Jamaica, left, and Kim Collins of Saint Kitts, right, during the men's 100 meter at the Diamond League track and field competition in Shanghai, China. Former 100-meter world-record holder Asafa Powell and Jamaican teammate Sherone Simpson have each tested positive for banned stimulants, according to their agent. Paul Doyle told The Associated Press on Sunday, July 14, 2013 that they tested positive for the stimulant oxilofrine at the Jamaican championships and were just recently notified. The news came the same day that American 100-meter record holder Tyson Gay revealed that he also failed a drug test. (AP Photo/Eugene Hoshiko, File)
Asafa Powell (kulia) akiwa na Nesta CarterPicha: picture alliance / AP Photo

Msemaji wa shirikisho la michezo ya riadha duniani IAAF Nick Davies amesema shirikisho hilo haliwezi kuzungumzia kuhusu kesi ambazo bado hazijaamuliwa , lakini ameongeza kuwa mapambano dhidi ya doping yameimarishwa , na sio kuporomoka , kila mara inapowezekana kufichua kesi mpya.

Wanariadha watano ikiwa ni pamoja na washindi wawili wa medali za olimpiki walipatikana na hatia ya kutumia madawa ya kutunisha misuli katika mashindano ya riadha nchini Jamaica .

Alcantara aja Ujerumani

Katika soka Mabingwa wa mataji matatu msimu huu Champions League, ligi ya Bundesliga na kombe la shirikisho la Ujerumani DFB Pokal Bayern Munich wamepata saini ya mchezaji wa kiungo Thiago Alcantara ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Uhispania kwa vijana wa chini ya miaka 21 ,na nyota chipukizi wa Barcelona. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amefunga mkataba na Bayern wa miaka minne hadi 2017 kwa kitita cha euro milioni 25, mabingwa hao wa Ulaya walithibitisha jana Jumapili(14.07.2013).

JERUSALEM, ISRAEL - JUNE 18: Thiago Alcantara of Spain poses with the trophy after winning the UEFA European U21 Championship final match against Italy at Teddy Stadium on June 18, 2013 in Jerusalem, Israel. (Photo by Alex Grimm/Getty Images)
Thiago AlcantaraPicha: Getty Images

Edinson Cavani yuko mjini Paris leo akikamilisha uhamisho wake kwenda Paris Saint-Germain, huku vyanzo ambavyo viko karibu na makubaliano hayo vikisema kuwa dau la euro milioni 64 litavunja rekodi ya uhamisho nchini Ufaransa.

Cavani mwenye umri wa miaka 26 mshambuliaji wa Napoli , ambaye aliweka wavuni mabao 29 katika ligi ya Italia , Serie A msimu uliopita amewasili mjini Paris leo.

[39246694] Napoli vs. InterMilan epa03689034 Napoli Edinson Cavani celebrates after he scores the 3:0 goal, during the Serie A soccer match Napoli vs InterMilan at san Paolo stadium in Naples, Italy, 05 May 2013. EPA/CIRO FUSCO +++(c) dpa - Bildfunk+++
Edinson CavaniPicha: picture-alliance/dpa

Pellegrini aonja kipigo

Manchester City inamatumaini ya kumpata mshambuliaji mpya kabla ya mwishoni mwa mwezi huu, amesema kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini jana baada ya timu yake kupokea kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya timu ya Afrika kusini ya SuperSport United katika mchezo wake wa kwanza akiwa kocha wa timu hiyo.

Timu hiyo iliyoshika nafasi ya pili katika Premier League msimu uliopita inataka kumpata mshambuliaji atakayechukua nafasi ya Carlos Tevez ambaye amejiunga na Juventus Turin na mchezo wao nchini Afrika kusini unaashiria haja ya kuwa na mshambuliaji mwingine.

Manchester City's Carlos Tevez in action against Wigan Athletic during their English Premier League soccer match at the City of Manchester Stadium, Manchester, England, Saturday Sept. 10, 2011. (AP Photo/Tim Hales)
Carlos TevezPicha: APImages

Arsenal London imekirarua kikosi cha kombaini ya Indonesia Dream Team kwa mabao 7-0 mwanzoni mwa ziara yao ya bara la Asia katika matayarisho ya timu hiyo. Nao mabingwa wa ligi ya Uingereza Manchester United ilipata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Singha All Stars mjini Bangkok chini ya kocha mpya David Moyes siku ya Jumamosi.

Nae kocha wa timu ya taifa ya Urusi Fabio Capello amekanusha uvumi juu ya uwezekano wa yeye kujiuzulu kutoka wadhifa huo, akisema kuwa anajisikia vizuri kabisa kufanyakazi Urusi, limeeleza gazeti la michezo la kila siku nchini humo.

Capello anaripotiwa kupokea ombi la kujiunga na mabingwa wa Ufaransa Paris Saint-Germain lakini majadiliano yalivunjika kuhusiana na masuala mbali mbali.

Mexico imekata tikiti yake katika robo fainali za michuano ya kombe la dhahabu Gold Cup katika mashindano yanayotayarishwa na shirikisho la kandanda la mataifa ya America ya kati na kaskazini CONCACAF kwa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Martinique, wakati Panama inasonga mbele kutoka kundi A baada ya sare ya bila kufungana na Canada.

Katika bara la Afrika shirikkisho la kandanda la Misri limependekeza kuwa mchezo wa Champions League kati ya mahasimu watani wa jadi kutoka mjini Cairo Zamalek na Al Ahly uchezwe katika mji wa kitalii ulioko katika eneo la bahari ya Sham wa El Gouna kwasababu za hofu ya usalama katika mji mkuu Cairo na mji wa bandari katika bahari ya Mediterranean wa Alexandria.

Hatua hiyo ya kuhamisha mchezo huo , ambao wenyeji ni Zamalek , haijaidhinishwa hata hivyo na shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF. Hata hivyo Zamalek imesema kuwa inafanya mipango kwa kikosi chake kwenda huko El Gouna siku ya Alhamis kabla ya Jumapili ambapo mchezo huo unatarajiwa kufanyika katika duru ya kwanza ya awamu ya timu nane zilizosalia katika kinyang'anyiro hicho.

Hali mbaya ya kisiasa nchini Misri pamoja na ghasia zilizofuatia kuondolewa madarakani kwa rais Mohammed Morsi kumesabaisha kuvurugika kwa kiasi kikubwa kwa ligi nchini humo.

Tanzania hoi

Matokeo ya mwanzo ya michuano ya kuwania kufuzu katika fainali za kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani ya nchi CHAN kati ya Tanzania na Uganda yanaonesha ishara ya kuondolewa na mapema kwa kikosi cha kocha wa Tanzania Kim Poulsen.

Timu ya taifa ya Tanzania pia haina nafasi katika michuano ya kuwania kufuzu katika fainali za kombe la dunia baada ya kupata kipigo dhidi ya Morocco na Cote D'Ivoire.

Kocha Poulsen hata hivyo anaeleza matumaini kuwa Taifa Stars inaweza kupata ushindi katika uwanja wa Nakivubo huko Uganda juma lijalo.

Mbio za Baiskeli - Tour de France.

Mwendesha baiskeli ambaye anapigiwa upatu kutoroka na taji la Tour de France msimu huu Chris Froome amesema leo kuwa anajisikia fahari kuiwakilisha Uingereza , licha ya kuwa alizaliwa na kukulia katika bara la Afrika.

Froome alizaliwa nchini Kenya na kuhamia nchini Afrika kusini akiwa kijana lakini anatambulika kama raia wa Uingereza kwasababu baba yake na babu zake walizaliwa nchini Uingereza na alianzia kupanda baiskeli katika timu ya Uingereza mwaka 2008.

Britain's Christopher Froome celebrates his yellow jersey of overall leader on the podium at the end of the 168.5 km ninth stage of the 100th edition of the Tour de France cycling race on July 7, 2013 between Saint-Girons and Bagnères-de-Bigorre, southwestern France. AFP PHOTO / JEFF PACHOUD (Photo credit should read JEFF PACHOUD/AFP/Getty Images)
Mwendesha baiskeli Christopher FroomePicha: Jeff Pachoud/AFP/Getty Images

Licha ya hivyo hakuwahi kuishi nchini Uingereza hadi pale aliposhindana katika Tour of Britain mwaka 2007 lakini amesema hana shaka kabisa juu ya uhusiano wake na nchi hiyo.

Wakati huo huo timu ya kiongozi huyo wa Tour de France Chris Froome imekubali kuweka wazi data zote za mazowezi pamoja na utendaji wake pamoja na data za damu ili kufanyiwa uchunguzi ili kuzima wasi wasi wowote wa kutumia madawa yanayoongeza nguvu, doping.

Mwandishi : Sekione Kitojo / ape / afpe / rtre

Mhariri: Yusuf , Saumu