1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gates ala kiapo kuongoza wizara ya ulinzi ya Marekani

18 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CBHs

WASHINGTON

Mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la Marekani CIA Roberts Gates anachukua rasmi wadhifa wa uwaziri wa Ulinzi wa Marekani, akimridhi Donald Rumsfeld aliyejiuzulu mwezi uliyopita.

Ggates anatarajiwa kula kiapo katika shughuli isiyo wazi kwenye Ikulu ya Marekani, kabla ya kuapa hadharani makao makuu ya wizara atakayoiongoza Pentagon.

Gates anachukua wadhifa huo mnamo wakati ambao kuna msukumo mkubwa wa akutaka kubadilishwa kwa sera za Marekani nchini Iraq.

Rais George Bush wiki iliyopita alisema kuwa atasubiri hadi mwezi ujayo kutangaza sera zake mbadala huko Iraq, akitoa nafasi ya kupata ushauri kutoka kwa waziri huyo mpya wa ulinzi.