1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gabon yajiandaa kwa AFCON

9 Januari 2017

Imebakia siku tano tu kabla ya kung'oa nanga dimba la Kombe la Mataifa ya Afrika – AFCON, na Gabon itakuwa mwenyeji wa tatu wa dimba hilo ambaye awali hakupewa kibali cha kuandaa tamasha hilo

https://p.dw.com/p/2VX6n
Polizist Angola Afrika
Picha: picture-alliance/dpa

Nafasi ya Libya ilichukuliwa na Afrika Kusini katika mwaka wa 2013 na Morocco ikajiondoa katika mwaka wa 2015 kutokana na hofu ya virusi vya Ebola hali iliyopiga fursa Guinea ya Ikweta kupewa kibali katika muda mfupi tu. machafuko yanayoendelea Libya yamefanya nchi hyo kujiondoa tena. Na hivyo kuwapa Gabon, fursa ya kuwa mwenyeji. Dimba hilo linang'oa nanga Januari 14 hadi Februri 5 katika maeneo manne ya mji mkuu Libreville, Port-Gentil, Frabceville na Oyem.

Timu ya Cote d'Ivoire ambayo ina mwonekano mpya itatetea taji lao la AFCON wakati mshambuliaji wa kasi zaidi wa wenyeji Gabon Pierre-Emerick Aubameyang anaongoza orodha ya majina ya wachezaji nyota. Majina mengine ni Riyad Mahrez wa Algeria na Sadio Mane wa Senegal. Studioni katika meza ya michezo niko na mwenzangu Sekione Kitojo kuzungumzia tamasha hili, Sekione, mashindano kama haya mara nyingi huwa na matokeo ya kushangaza lakini ni timu gani unazohisi zina nafasi kubwa?

Mwandishi: Bruce Amani/AFPDPA
Mhariri:Yusuf Saumu