1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gabon yaaga mashindano ya Afcon

Sekione Kitojo
23 Januari 2017

Wenyeji  wa  mashindano  ya  fainali  za  kombe  la  mataifa  ya Afrika  Gabon  waaga  mashindano, Senegal, Burkina Faso, na Cameroon  zatinga  robo  fainali , Tunisia matumaini  ni  makubwa katika  kundi  B.

https://p.dw.com/p/2WGWx
Fußball | Africa Cup 2017 | Gabun vs Guniea Bissau | Team Gabun
Kikosi cha timu ya taifa ya Gabon katika kombe la mataifa ya Afrika AfconPicha: picture-alliance/abaca/C. Liewig

 

Huko  mjini  Libreville  ambako  timu  16  za  mataifa  ya Afrika  zinawania  ubingwa  wa  mataifa  hayo  katika  kombe  la Afrika , ambapo  jana  Jumapili  kundi  A lilimaliza  michezo  yake  na wenyeji  wa  mashindano Gabon kuaga  mashindano  hayo  baada ya  kutoka  sare  tasa  dhidi  ya   Simba  wa  nyika  Cameroon.

Guinea Bissau  ilikubali  kipigo  cha  mabao  2-0  dhidi  ya  Burkina Faso  na  hivyo  Burkina  Faso  kutinga  katika  robo  fainali  pamoja na Cameroon. 

Afrika Cup Algerien Tunesien
Wachezaji wa timu ya Tunisia wakishangiria baoPicha: Reuters

Jumatatu kutakuwa  na  mpambano  kati  ya  Zimbabwe ikipambana  na  Tunisia wakati  huo  huo Senegal ikipambana  na  Algeria.

Kuna  hali  ya  wasi  wasi  mkubwa  kuhusiana  na  ubora  wa viwanja  katika  mashindano  haya  ya  Afcon. Hali  hii  inaelezwa kuwa  imechangia  kuzorotesha  ubora  wa  michezo  hiyo  na  ukame wa  mabao  pia  huku  wachezaji   hasa  wanaocheza  soka  ya kulipwa  katika  mataifa  ya  Ulaya wakicheza kwa  tahadhari  kubwa. 

 

Mwandishi:  Sekione  Kitojo / afpe / dpae /  rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahhman