1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gündogan atafakari kuondoka Dortmund

11 Januari 2016

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Ilkay Gündogan hajausaini mkataba wa muda mrefu na Borussia Dortmund wakati kiungo huyo akitafakari ikiwa ataongeza mkataba wake utakaokamilika 2017 au ahamie katika klabu mpya

https://p.dw.com/p/1HbUS
Fußball Bundesliga 2014/2015 VfB Stuttgart Borussia Dortmund
Picha: picture-alliance/dpa/Ronald Wittek

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa katika klabu ya Dortmund tangu 2011, alidokeza mwaka jana kuwa angeondoka huku vilabu kadhaa nchini Italia na Premier League ya England vikimtaka, kabla ya kusaini mkataba mpya wa miaak miwili mwezi Julai.

Gündogan ameliambia gazeti la Bild leo kuwa hajafanya uamuzi wowote na lazima atathmini kila kitu kwa sababu urefu wa taaluma ya mtu una ukomo. Ameongeza kuwa kila kitu kingali wazi, na kuwa mkataba wake ujao utakuwa mrefu na sio wa mwaka mmoja tu. Dortmund kwa sasa wako katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Bundesliga.

Kiessling nusra aihame Leverkusen

Mshambuliaji wa zamani wa Ujerumani Stefan Kiessling alikuwa karibu kujiunga na Hanover katika kipindi hiki cha uhamisho, kabla ya kuamua kusalia katika Bayer Leverkusen.

Fußball Bundesliga Bayer Leverkusen - Borussia Mönchengladbach
Mshambuliaji wa Leverkusen Stefan KiesslingPicha: Getty Images/Bongarts/S. Steinbach

Kiessling ameliambia gazeti la Bild leo kuwa nusra ahame baada ya kukasirishwa na sehemu ya kwanza ya msimu ambao mchezaji aliyesainiwa Javier “Chicharito” Hernandez aling'ara katika safu ya mashambulizi.

Anasema alikwenda Hanover, maana kulikuwa na ombi la kumtaka. Kiessling mwenye umri wa miaka 31 anamfahamu kocha wa Hanover Martin Bader kutoka klabu ya Nüremberg. Licha ya kutoanza mechi nyingi, Amefunga magoli matatu pekee katika Bundesliga, ikilinganishwa na 11 ya Hernandez. Amesema atafanya mazungumzo na uongozi wa Leverkusen mwishoni mwa msimu kabla ya kuchukua uamuzi wowote.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA
Mhariri: Mohamed Khelef