1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fuko jipya la kinga ya Euro laidhinishwa Copenhagen

30 Machi 2012

Mawaziri wa fedha wa kanda ya Euro wakubaliana baada ya majadiliano makali liundwe fuko jipya na kubwa zaidi badala ya lile la zamani,kuimarisha utulivu wa sarafu ya Euro.

https://p.dw.com/p/14VRj
Mawaziri wa kanda ya EuroPicha: Reuters

Mawaziri wa fedha wa kanda ya Euro wamekubaliana mjini Copenhagen kuzidisha kiwango cha fedha kuzuwia kutokea tena mgogoro wa madeni.Jumla ya Euro bilioni 800 zitahitajika kuzuwia masoko ya fedha yasibahatishe dhidi ya Hispania na Italy.Hadi wakati huu Ureno, Ireland na Ugiriki ndizo zinazopatiwa mikopo ya dharura kutoka mataifa ya kanda ya Euro na shirika la fedha la kimataifa IMF.

Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano,maridhiano yameweza kupatikana mjini Copenhagen.Hata hivyo hesabu zilizotolewa zinatatanisha.Dhahiri ni kiwamba kuanzia msimu wa kiangazi pataundwa fuko jipya na la kudumu la kuhifadhi sarafu ya Euro kwa jina "Mkakati wa kuleta utulivu-ESM-Fuko hilo linatarajiwa kuwa na fedha taslimu zisizopungua Euro bilioni 500 ambazo nchi zinaweza kukopa ikihitajika.Fedha hizo zitakuwa zikiongezeka kidogo kidogo kwakua mataifa wanachama yatakuwa yakichangia fedha taslimu ili kuleta utulivu katika shughuli za kutoa mikopo.

Mpango wa awali wa kuiokoa sarafu ya Euro,nafasi yake itachukuliwa na huu wa sasa wa ESM.Kiwango cha fedha za mikopo hapo awali kilikuwa Euro bilioni 440.Halmshauri kuu ya Umoja wa Ulaya,Ufaransa na mataifa kadhaa ya kanda ya Euro wanataka taasisi hizo mbili za fedha zichanganywe.Kwa namna hiyo kiwango jumla cha fedha kitakuwa Euro bilioni 940 kwa hivyo masoko ya fedha yatatulia.

Wolfgang Schäuble Jean-Claude Juncker
Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schäuble na mwenyekiti wa kanda ya Euro Jean-Claude JunckerPicha: dapd

Waziri wa fedha wa Ufaransa Francois Baroin analinganisha faida ya fuko kama hilo na kitisho cha bomu la atomiki katika enzi za vita baridi.Waziri wa fedha wa serikali kuu ya Ujerumani Wolfgang Schäuble hakuwa tayari bado kuunga mkono fuko kubwa kama hilo.Ujerumani-dola kuu la kiuchumi katika kanda ya Euro,inabidi itoe dhamana kubwa zaidi.Hata hivyo waziri Wolfgang Schäuble alionyesha yuko tayari kuunga mkono maridhiano ili kuepukana na mvutano miongoni mwa nchi wanachama wa kanda ya Euro."Tunakutana ili tujadiliane.Kuna maoni tofauti.Mtu anaweza kuyalinganisha na mvutano.Lakini daima tunafikia ufumbuzi.Ni kutokana na hisia za kuaminiana na kwa lengo la kutafuta ufumbuzi wa pamoja." Amesema waziri wa fedha wa Ujerumani.

Wolfgang Schäuble na waziri mwenzake wa Finnland Jutta Urpilainen wameunga mkono fuko la awali la mkopo lililokuwa na Euro bilioni 200 lichanganywe na fuko jipya la ESM na kuwa na jumla ya Euro bilioni 700.Schäuble amehesabu pia Euro bilioni 100 kutoka halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya na mikopo kutoka fuko la misaada kwa Ugiriki na kwa namna hiyo kufikia kiwango cha Euro bilioni 800.

Eurogruppe EU Finanzminister Treffen Brüssel Juncker
Waziri mkuu wa Luxembourg Juncker akizungumza na waandishi habariPicha: dapd

Hesabu hizo ndizo zilizokubaliwa hatimae.Pindi Italy ikitumbukiya nayo katika mgogoro,Euro bilioni 240 kutoka fuko la zamani la kuinusuru sarafu ya Euro zinaweza kutumiwa na kwa namna hiyo kulifanya fuko jipya kuwa na kitita cha karibu Euro bilioni 1000.

Mwandishi:Riegert,Bernd/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Mohammed Abdul-Rahman