FREE TOWN: Zoezi la kuhesabu kura laendelea | Habari za Ulimwengu | DW | 12.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

FREE TOWN: Zoezi la kuhesabu kura laendelea

Shughuli za kuheasabu kura zianaendelea nchini Sierra Leone baada ya taifa hilo la Afrika Magharibi kufanya uchaguzi wa kwanza wa urais na bunge hapo jana tangu majeshi ya umoja wa mataifa ya kulinda amani yalipo ondoka kutoka nchini humo.

Wasimamizi wa uchaguzi wa umoja wa ulaya wamesema kwamba wameridhishwa na zoezi la kupiga kura ambalo lilifanyika kwa amani.

Mgombea wa chama cha upinzani cha Peoples Congress Ernest Koroma ni mpinzani mkubwa wa makamu wa rais na mgombea wa chama tawala cha Sierra Leone People’s Party Solomon Berewa katika kinyang’anyiro cha kiti cha rais.

Idadi kubwa ya wapiga kura walishiriki katika uchaguzi huo wa jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com