1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Free Town: Wakuu wawili wa uasi wapatikana na hatia ya uhalifu wa kiviti nchini Sierra Leone.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcp

Mahakama ya Umoja wa Mataifa ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone imewapata na hatia ya uhalifu wa kivita wakuu wawili wa kundi la wapiganaji lililounga mkono serikali.

Hata hivyo mahakama hiyo imewaachia huru wakuu hao kwa makosa makuu ya uhalifu dhidi ya binadamu.

Viongozi hao walikuwa wakiongoza kundi la wapiganaji la Civil Defence Forces lililokuwa likipigana kwa niaba ya Rais Ahmad Tejani Kabbah wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya kati ya mwaka 1991 na mwaka 2002.

Allieu Kondewa na Moinina Fofana walikuwa wameshtakiwa kwa makosa manane ya uhalifu dhidi ya binadamu, uhalifu wa kivita na makosa mengine likiwemo kosa la kuajiri askari watoto.

Washtakiwa hao wawili hawakupatikana na hatia ya mauaji wala uhalifu dhidi ya binadamu.