1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Free Town. Tony alakiwa kishujaa.

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwR

Waziri mkuu wa Uingereza anayeondoka madarakani Tony Blair, ambaye yuko nchini Sierra Leone , ameyataka mataifa ya magharibi kuongeza fedha na misaada mingine kwa jeshi la Afrika la kulinda amani.

Katika mkutano na waandishi wa habari pamoja na maraisa wa Sierra Leone na Liberia, Blair amesema kuwa mataifa ya magharibi yamehakikisha kuwa umoja wa Afrika unapata vifaa vya kutosha kuweza kuingilia kati katika mizozo na kusaidia majanga ya kiutu ambayo yanatokea katika ardhi ya Afrika.

Blair alilakiwa kama shujaa wakati akiwasili katika taifa hilo la Afrika magharibi kutokana na hatua yake ya kutuma majeshi katika koloni hilo la zamani la Uingereza May 2000 wakati waasi wakikaribia katika mji mkuu Free Town wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.