1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FRANKFURT:Deutsche Telekom yaruhusiwa kufanya mabadiliko

1 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCNY

Bodi ya usimamizi ya kampuni ya simu ya kitaifa ya Ujerumani Deutsche Telekom inapuuza maandamano ya wafanyikazi na kupewa ruhusa ya kuendelea na mpango mzima wa kufanya mabadiliko.Kampuni hiyo inapanga kuanzisha idara mpya ya T-Service itakayowahusisha wafanyikazi alfu 45 watakaohudumu kwa masaa mengi zaidi na mshahara mdogo zaidi.Deutsche Telekom inatetea hatua hiyo mpya ya kupunguza nafasi za kazi vilevile mabadiliko ili kuweza kushindana na kampuni nyingine.

Deutsche Telekom iliyoko hapa mjini Bonn ilipata faida ya euro milioni laki tisa mwaka uliopita ikilinganishwa na hasara katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka jana.

Kulingana na wadadisi waliochambua taarifa za Dow Jones,kampuni hiyo ilitarajiwa kupata faida ya euro milioni laki sita.Hasara hiyo inadhaniwa kusababishwa na upungufu wa wateja wa simu za ndani vilevile kupunguzwa kwa nafasi za kazi.