FRANKFURT YAUMANA LEO NA STUTTGART | Michezo | DW | 16.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

FRANKFURT YAUMANA LEO NA STUTTGART

Viongozi wa Bundesliga Schalke wanarudi uwanjani kesho kuumana na Wolfsburg wakati jioni hii vumbi litawaka kati ya Frankfurt na Stuttgart.Amerika Kusini inajiwinda tayari kwa kombe la dunia 2010.

Firimbi italia Septemba 10 mwaka huu kwa timu za Amerika kusini kuania nafasi zao kwa kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini, la kwanza barani Afrika.

Schalke ikiongoza kileleni mwa Bundesliga imerefusha na mapema mkataba wa kocha wake -Mirko Slomka.Frankfurt inafungua duru ya mwishoni mwa wiki hii ya Bundesliga, ikiwa na miadi ijumaa hii na Stuttgart.

Kombe la dunia 2010:ingawa lipo mbali mno,firimbi kwa timu za kanda ya Amerika kusini, italia Septemba 8 mwaka huu kunyan’ganyia nafasi 4 au 5 za bara hilo nchini Afrika Kusini.Baada ya kikao chake huko Caracas Venezuela,kamati-tendaji ya shirikisho la dimba la huko lililopiga kura jana juu ya Copa America, liliamua pia kuandaa mechi 2 kwa wiki wakati wa kinyan’ganyiro hicho cha tikiti za kombe la dunia.

Kanda ya Amerika kusini ina nafasi 4 wazi na zaweza kuongezeka kuwa 5.

Shabani nionda wa jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ameungama kwamba itambidi kuonesha ustadi wake zaidi ikiwa ajipatie nafasi ya kudumu katika kikosi cha Blackburn Rovers ya Uingereza anachokichezea:

Nonda alieazimwa kutoka Roma ya Itali kwa msimu huu, ndie alietia bao la pili la Rovers juzi katika mpambano na Bayer Leverkusen uliomalizikia ushindi wa mabao 3:2 wa Leverkusen.

Tayari Shabani Nonda akishirikiana na muafrika kusini Benni McCarthy wametia mabao 21 msimu huu wakiichezea Blackburn Rovers.

Kufuatia changamoto za jana Newcastle,Sevilla na Lens zaonesha ziko njiani kuingia duru ijayo ya kombe la ulaya la UEFA.Zote zilishinda kwa vishindo mapambano yao ya jana.New Castle ilitia mabao 3-1 katika kipindi cha pili jana ndani ya lango la Zulte-Waregem ya Ubelgiji.

Lens pia ya Ufaransa ilikomea mabao 3-1 katika lango la Panathniakos ya ugiriki huku staid wa Tunisia Issam Jamaa akipiga hodi langoni mara 2 na kukaribishwa karibu.

Bundesliga-ligi ya Ujerumani inarudi uwanjani jioni hii kwa mpambano kati ya Frankfurt na Stuttgart.

Kesho ijumamosi Alemaania Aachen itaumana na mabingwa Bayern Munich wakati Werder Bremen iliotamba majuzi katika UEFA CUP ikicheza na Hamburg.Wolfsburg ina miadi na vionmgozi wa Ligi Schalke ambao punde hivi wameonesha shukurani zao kwa kocha wao:

Kocha Mirko Slomka amerefushiwa mkataba wake kabla ya changamoto hiyo ya kesho na Wolfsburg.Borussia Dortmund inacheza na Borussia Monchengladbach wakati Hertha Berlin inataka kutamba mbele ya Mainz.Bayer Leverkusen ilioitoa Blackburn Rovers katika UEFA cup juzi ina miadi na Hannover.

Jumapili duru hii ya Bundesliga itakamilishwa kwa zahama kati ya Armenia Bielefeld na Bochum na Energie Cottbus na Nüremberg.